MICHEZO

DIAMOND ATANGAZA KUFUNGA NDOA NA WEMA
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.

“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.




Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.

“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.

“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”

Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”

Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’ alisema: “Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.

Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.

“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.

Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi kujibishana.

“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
“Lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa sisi ndio tunaoujua ukweli wa uhusiano wetu.

“Sidhani kama ni sahihi mapenzi yetu yakawa na wasemaji wengine zaidi yetu wenyewe. Sasa ni ajabu watu wanaposema yao.


_____________________________________________________________________________
HISTORIA YA MAREHEMU KANUMBA
Steven Charles Kanumba (8 Januari 1984, Shinyanga – 7 Aprili, 2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Maisha
Steven alianza masomo yake katika shule ya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.

Shughuli za uigizaji
Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya “90″. Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.

Hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.

Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to Lagos, She is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.  
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.










Filamu na Tamthilia Alizotunga. 1 Tufani ( Johari )
2 Gharika
3 Baragumu
4 Sikitiko Langu
5 Johari 2
6 Dangerous Desire
7 Dar 2 Lagos
8 Cross my Sin
9 Village Pastor
10 Family Tears Filamu na Tamthilia Alizoigiza 1 Jahazi ( Tamthilia )
2 Dira ( Tamthilia )
3 Tufani ( Johari )
4 Gharika( Tamthilia )
5 Baragumu( Tamthilia )
6 Sikitiko Langu ( Filamu )
7 Johari 2 ( Filamu )
8 Dangerous Desire ( Filamu )
9 Dar 2 Lagosi
10 Riziki ( Filamu ) 11 Cross my Sin( Filamu )
12 Uncle JJ (Filamu)
Na nyinginezo nyingi sana……
Steven Kanumba alitangaza hivi karibuni nia ya kuwa mgombea wa ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi. Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasnia ya filamu Tanzania na Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Mwenyezi mungu amuweke pema na penye nuru…..Amen.!
__________________________________________________________________________________
MAXIMO ATUA YANGA
YANGA imemtambulisha rasmi kocha wake mpya, Marcio Maximo kisha akatamka kwamba atafanya mambo ya kisasa Afrika itaitambua Yanga.

Sambamba na hilo, mido mpya wa timu hiyo Mbrazili Andrey Coutinho naye amewasili tayari kuongeza makali ya wana Jangwani hao.

Akizungumza katika mkutano wa utambulisho wake, Maximo alisema baada ya kufanikiwa kurudi Tanzania sasa anataka kuhakikisha katika miaka miwili Yanga inarudisha heshima yake.
“Nawashukuru viongozi wa Yanga kwa nguvu yao ya kuhakikisha narudi Tanzania, walionyesha kunielewa kila tulipokuwa tunajadiliana, kazi yangu hapa si uwanjani pekee nataka Yanga iwe ya kisasa zaidi,”alisema kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars.

“Sasa tunatakiwa kushirikiana kwa kila jambo, nataka kila kitu hapa kiendeshwe kwa kufuata taaluma nimepata taarifa kuwa ushindani katika ligi hapa umeongezeka, nataka jambo moja kubwa lifanyike nikiwa hapa ambalo ni kurudisha heshima ya timu hii.”

Awali Katibu Mkuu wa Yanga Beno Njovu akizungumza katika utambulisho huo alisema Maximo amepewa vyeo viwili ambavyo ni Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Mkuu.

“Uongozi wetu umedhamiria kwa dhati kuhakikisha sasa mkazo mkubwa unawekwa katika soka la vijana na hili sio siasa kuendesha timu ya vijana pia atakuwa akisaidiana na msaidizi wake Leonardo Neiva.
 








Awasamehe Kaseja,Chuji
Kama vile alijua kuwa watu wanasubiri kujua nini hatma ya mgogoro wake na kipa wa timu hiyo Juma Kaseja, Maximo alisema yaliyotokea baina yake na kipa huyo mkongwe wakiwa  Taifa Stars ni historia na anafungua ukurasa mpya sawa na kwa  kiungo Athuman Idd ‘Chuji’ japo sasa hayupo Yanga.
“Haya ni maisha mapya,  nafurahi kuikuta Yanga ikiwa na makipa bora watatu;  Dida (Deogratias Munishi), Kaseja na Barthez (Ally Mustapha),”alisema Maximo huku akionyesha furaha usoni.
Akizungumzia ushindani wa ligi Maximo alisema: “Miaka minne iliyopita wakati naondoka hapa nilitaka kuona ushindani katika klabu unaongezeka sasa nimeambiwa kuna Mbeya City na Azam, nataka Yanga iwe juu yao, nawaheshimu Simba.”
Katika kuhakikisha Maximo anayafanya kwa usahihi majukumu yake uongozi wa Yanga umethibitisha kumtafutia uwanja mzuri wa mazoezi ambapo tayari kocha huyo ameeleza kuwa anataka kuanza na kuimarisha stamina kabla ya kugeukia ufundi uwanjani kazi ambayo ataianza keshokutwa Jumatatu.






No comments:

WELCOME TO SEEISSAI BLOG