SIASA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi katibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo.
Siku moja baada ya makamu wa rais dkt mohamed ghalib bilal kuhimiza mahusiano mema wakati wa utendaji kazi baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vya habari, jeshi la polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa limekiuka kauli hiyo kwa kuwapiga na kuwajeruhi baadhi ya waandishi wa habari na kuwazuia kutekeleza wajibu wao wakati mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema alipowasili katika makao makuu ya jeshi hilo kwa mahojiano.
Kauli hiyo ya makamu wa rais imeshindwa kutekelezwa kutokana na tukio lililotokea majira ya saa 5 na dk 15 asubuhi wàkati mwenyekiti wa chadema taifa Mhe. Freeman Mbowe alipowasili makao makuu na askari wa polisi  kutaka kuzuia gari alilopanda kuingia ndani ya lango kuu pamoja na waandishi wa habari na watu wengine kuamriwa kuondoka katika eneo hilo agizo lililopingwa na waandishi wa habari na baadhi ya wanasheria wa Chadema.
Kufuatia na kutolewa kwa ilani hiyo jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia-FFU- kilianza kupiga waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wananchi huku wengine wakikimbia kuhofu vipigo toka kwa askari hao ambapo baaadhi ya waandishi walioumizwa sehemu mbalimbali ya mihili yao.
Akiwatangazia wafuasi waliokuwa wakikataa kuondoka katika maeneo hayo mwanasheria wa chadema mhe. Tundu lissu licha ya kuwahakikishia kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa Mhe. Freeman Mbowe yuko salama amewataka kuondoka katika eneo hilo na kurudi majumbani ili kuepusha vurugu na misongamano ambayo ingeweza kusababisha matatizo zaidi.
Aidha ITV imeshuhudia mwenyekiti wa Chadema taifa Mhe Freeman Mbowe akitoka makao makuu ya jeshi la polisi akisindikizwa na ulizni mkali wa jeshi la polisi kuelekea katika ofisi za makao makuu ya chama hicho baada ya kukamilika kwa taratibu za kipolisi



 Wafuasi wa Chadema wakimsindikiza mwenyekiti wao Freeman Mbowe kuelekea Makao makuu ya jeshi la polisi

 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Jeshi
 Huyu alikuwa akikaidi amri ya Jeshi la Polisi ilibidi aondolewe kwa nguvu.


Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la Polisi.

------------------------------
Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Dr Ali Mohamed Shein Unguja

  Viongozi mbalimbali wachama cha Mapinduzi wakiwa katika Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM huko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar

  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohd Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama hicho na Wananchi mbalimbali waliokwenda kumpokea hapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar.

 Msafara wa Wapanda Pikipiki wa Chama cha Mapinduzi ukiwa mbele katika Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohd Shein ukitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar.

 Msafara wa Wapanda Pikipiki wa Chama cha Mapinduzi ukiwa mbele katika Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohd Shein ukitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar.

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohd Shein akiwapungia Mkono Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar 

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohd Shein (watatu kulia)akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Dini na Chama katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amaan Karume ili kumuombea Dua Rais huyo mara baada ya kufika katika Makao Makuu ya Chama hicho Kisiwa Ndui Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohd Shein akitoa hotuba kwa Wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliofika Mkao Makuu ya Chama ili Kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake huko Dodoma na kumtakia kheri katika Kuiongoza Zanzibar.
______________________________________________________________

POLISI YAZIMA MAANDAMANO YA CHADEMA
Jeshi la polisi mkoani Dodoma leo limezima maandamano yaliyopangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupinga kuendelea kwa vikao vya Bunge la Katiba kwa kile wanachodai ni kufuja fedha za umma.

 Maandamano ya CHADEMA Mkoa wa Dodoma yamedhibitiwa kwa Mkoa mzima.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) (pichani) amesema katika hilo kuna gari lenye namba za usajili T.792 CAX aina ya Pick up Ford Ranger nyeupe mali ya CHADEMA iliyokuwa ikiendesha na CHRISTOPHER NYAMWINJA, Mweneye miaka 52, Mgogo, Mkristo Mratibu wa CHADEMA Kanda ya magharibi ambapo makazi yake ni TABORA mjini limekamatwa mtaa wa KUU karibu na kituo cha mafuta cha GAPCO...

CHADEMA iliyokuwa ikiendesha na CHRISTOPHER NYAMWINJA, Mweneye miaka 52, Mgogo, Mkristo Mratibu wa CHADEMA Kanda ya magharibi ambapo makazi yake ni TABORA mjini limekamatwa mtaa wa KUU karibu na kituo cha mafuta cha GAPCO jirani na WIMPI RESTAURANT likiwa na watu wengine watatu ambao ni:-
1.     LAURENT S/O MANGWESHI mwenye miaka 36, Mkristo, Msukuma Mkulima wa Wialya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
2.     AGNES D/O STEPHANO mwenye miaka 26, Mhehe, Mkristo Mfanyabiashara Mkazi Ubungo MAziwa Dar es Salaam.
3.     ELISHA S/O DAUDI mwenye miaka 49, Msukuma, Mkristo Fundi umeme Mkazi wa TAbora.
Kamanda LUKULA – ACP amesema gari hilo lilikuwa na bango lenye maandishi “TUNAPINGA UFISADI UNAOFANYWA NA BUNGE LA KATIBA”. Likiwa na maandishi ubavuni mbele na nyuma M4C.
Aidha Kamanda LUKULA – ACP ameongeza kuwa kabla ya kukamatwa kwa gari hilo Polisi walilikimbiza na katika kupita kwenye kona/mtaa watu wawili waliruka kutoka kwenye gari hilo na kukimbia kusikojulikana na bango hilo. Watu waliobaki ndani ya gari hilo ambao ni wanne ndio waliokamatwa.Askari Polisi wakiwa kwenye zoezi la kuzuia Maandamano ya Chadema Mjini Dodoma



_________________________________________________________________________________________
YALIYOJIRI BUNGENI MARA BAADA YA MWANASHERIA WA SEREKALI YA ZANZIBAR KUPINGA BAZI YA VIFUNGU
 Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akipiga kura leo kwenye ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kupitisha Sura na Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Yahya Kassim Issa akiomba mwongozo leo Bungeni kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kuhusu kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman kuja kupiga kura na kukataa baadhi ya Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa wakati alijitoa kwenye Kamati ya Uandishi ambapo alitakiwa awepo akitetea maslahi ya Zanzibar, jambo ambalo limewachanganya baadhi ya wajumbe



 Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar.




No comments:

WELCOME TO SEEISSAI BLOG