RAISI KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA MWENGE TEGETA
Muonekano wa Barabara ya Mwenge Tegeta.
Rais Jakaya Kikwete aka na Balozi wa Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada katika hafla ya uzinduzi barabara hiyo.
Rais Jakaya Kiwete akiwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki
Okada pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua barabara ya
Mwenge -Tegeta.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada leo wamezindua barabara ya Mwenge Tegeta yenye urefu wa kilomita 12.9.
Uzinduzi wa barabara hiyo umefanyika katika eneo la Lugalo Mwenge jijini Dares salaam.Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada wakizundua barabara hiyo.
________________________________________________________________________________________
KABURI LA MTOTO SHAABAN MAULID ALIYEFARIKI KISHA KUONEKANA AKIWA HAI ZAIDI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA LAFUKULIWA KWA AJILI YA UCHUNGUZI
_______________________________________________________________________________________
MAJOZI MAKUBWA ZANZIBAR BAADA YA MELI KUZAMA KATIKA MKONDO WA NUNGWI
Raisi wa ZANZIBAR na mwenyekiti wa barala la mapinduzi Dk Ally Mohamed Shein wakiw ana huzuni nzito baada ya kuwasili sehemuya tukio la ajali ya meli ya Mv spice mapema leo
__________________________________________________________________________________
MAZISHI YA SHEKHA NASOR BACHU
Inna lillahi wa inna ilaihi rajiun!
Kwa taarifa za kuaminika hii leo zinaeleza kuwa sheikh Nassor Bachu amefariki hii leo. Sheikh alianza kuugua ghafla kwa kupata stroke na baadaye kuendelea kujiuguza nyumbani kwake huku akizuiwa kudarsisha chochote kutokana na hali yake kiafya. Kwa kipindi cha kama mwaka hivi hali yake ilizidi kuwa mbaya na kubakia kuuguzwa kitandani tu na hivyo akapelekwa India mwishoni mwa mwaka 2012 kwa matibabu na kuelezewa kuwa ana mgando wa damu ndani ya ubongo wake. Tiba haikuwepo kwa hali hiyo na hivyo kurejeshwa nchini na kuendelea na dawa za kawaida.
Sheikh aliwahi kuzushiwa kifo sio chini ya mara tatu na kusababisha mwanawe kuanza kutoa taarifa katika vyombo vya habari ikiwemo redio imani kuwa ni habari za uzushi na wala familia haijapata kuomba msaada wa mchango wa matibabu.
Maziko yatakuwa kesho (14/02/2013) saa nne asubuhi Chukwani (wanawake), kusaliwa ni Masjid Sunna Kikwajuni na kuzikwa Donge – Unguja inshallah.
MOLA AMSAMEHE MADHAMBI YAKE, AMJAALIE KAULU THABIT NA AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI.
_________________________________________________________________________________________
RAIS DKT. KIKWETE ASIMIKWA UCHIFU WA KABILA LA WABENA MKOANI NJOMBE
________________________________________________________________________________________
____________________________________________________________________________________
MABOMU NDANI YA DARAJANI

SIKU chache baada kulipotiwa tukio la mtoto Shaban Maulid (15)
anayedaiwa kufariki miaka miwili iliyopita na kuonekana tena akiwa hai,
hivi karibuni,kaburi lake anakodaiwa kuzikwa sasa lafukuliwa kwa ajili
ya uchunguzi wa kitaalam wa DNA
Tukio la kufukua kaburi
hilo lilifanyika Jana 03.10.213 majira saa 08:30 asubuhi na kusababisha
shughuli za kawaida katika mji wa Geita na mitaa yake kusimama kwa muda
kwa ajili ya wakazi wa maeneo hayo kwenda kushuhudia tukio hilo
lililostaajabisha wengi.
Ilipofika majira ya saa moja
na nusu asubuhi watu walianza kumiminika nyumbani kwa baba wa mtoto
aliyefariki kisha kuonekana na ilipofika majira ya saa mbili maofisa wa
jeshi la polisi Mkoani hapa wakiambatana na mtaalamu kutoka ofisi ya
mkemia mkuu kanda ya ziwa waliwasili eneo hilo.
Aidha
zoezi hilo lilifanyika kwa amani baada ya askari polisi waliovalia sare
na makachero kuimarisha ulinzi eneo hilo ambapo mamia ya wakazi wa Geita
mjini na wale wa maeneo ya jirani kufurika eneo hilo kushuhudia tukio
zima.
Akizungumza mara baada ya kufukua mabaki hayo
mkemia huyo kutoka ofisi ya Kanda Lucas Ndunguru alisema wamechukua
mifupa miwili mirefu kutoka kwenye miguu yote miwili kwa ajili ya kwenda
kupima ili kupata ukweli halisi .
Mtaalamu huyo
alisema lengo ni kutaka kujua mtoto aliyepatika kama ndiye mtoto wao
halisi pamoja na kujua kilichokuwa ndani ya kaburi hilo,ambapo alisema
tayari wazazi wote wamechukuliwa vipimo vya DNA kwa ajili ya kupate
ukweli halisi huku akisema wanatarajia baada ya wiki mbili watakuwa
wamepata majibu .
"tunakwenda kuchunguza sasa,tayari
wazazi wote tumeshachukua vipimo vyao na vile vya mtoto,hatua inayofuata
ni kuchunguza na hii mifupa tuliyoichukua kwa ajili ya kulinganisha na
baada ya hapo ukweli utapatikana" alisema Lucas
Hata
hivyo wakati wakiendelea kufukua kaburi hilo walipofika urefu wa futi
moja na nusu walikutana na chungu ambacho ndani yake kulikuwa na mifupa
ilisadikiwa kuwa ni ya kuku na kuleta mshangao mkubwa kwa watu .
Mtoto
huyo Maulidi Shaban alionekana amefariki ndani ya kisima cha maji
Tarehe 01.01.2011 baada kwenda kuchunga Mbuzi kisha kushindwa kurudi
nyumbani na baadaye kuonekana baada ya siku tatu akiwa amefia kwenye
kisima.
Septemba 30 mwaka huu.mtoto huyo alikutana ana
kwa ana na mama yake mzazi Aziza Ramadhan wakati maeneo ya maeneo ya
mtaa Mwembeni akitambuliwa kwa kila kitu na wazazi wake hata majirani na
walimu wa mtoto huyo wote wakisema ni yeye bila kutia shaka.
Mtoto
huyo aliyekuwa akisoma darasa la tano mwaka huo kwa sasa hajaweza
kuongea vizuri ambapo kwa mujibu wa daktari wa hospitali ya wilaya
Dr.Adamu Sijaona alisema mtoto huyo ataendelea kuwepo hospitalini hapo
kwa uchunguzi zaidi wa kiafya ambapo alisema anaendelea vizuri.
Ofisi
ya Polisi Mkoani Geita ambayo inafuatilia tukio hili kwa karibu hapa
imeendelea kuwaomba wananchi kuendelea kusubiri majibu ya Mkemia mkuu
ambapo wananchi hao walitaka kupata majibu siku ya Jana ya kufukua
kaburi hilo
_______________________________________________________________________________________
MAJOZI MAKUBWA ZANZIBAR BAADA YA MELI KUZAMA KATIKA MKONDO WA NUNGWI
Raisi wa ZANZIBAR na mwenyekiti wa barala la mapinduzi Dk Ally Mohamed Shein wakiw ana huzuni nzito baada ya kuwasili sehemuya tukio la ajali ya meli ya Mv spice mapema leo
__________________________________________________________________________________
MAZISHI YA SHEKHA NASOR BACHU
Inna lillahi wa inna ilaihi rajiun!
Kwa taarifa za kuaminika hii leo zinaeleza kuwa sheikh Nassor Bachu amefariki hii leo. Sheikh alianza kuugua ghafla kwa kupata stroke na baadaye kuendelea kujiuguza nyumbani kwake huku akizuiwa kudarsisha chochote kutokana na hali yake kiafya. Kwa kipindi cha kama mwaka hivi hali yake ilizidi kuwa mbaya na kubakia kuuguzwa kitandani tu na hivyo akapelekwa India mwishoni mwa mwaka 2012 kwa matibabu na kuelezewa kuwa ana mgando wa damu ndani ya ubongo wake. Tiba haikuwepo kwa hali hiyo na hivyo kurejeshwa nchini na kuendelea na dawa za kawaida.
Sheikh aliwahi kuzushiwa kifo sio chini ya mara tatu na kusababisha mwanawe kuanza kutoa taarifa katika vyombo vya habari ikiwemo redio imani kuwa ni habari za uzushi na wala familia haijapata kuomba msaada wa mchango wa matibabu.
Maziko yatakuwa kesho (14/02/2013) saa nne asubuhi Chukwani (wanawake), kusaliwa ni Masjid Sunna Kikwajuni na kuzikwa Donge – Unguja inshallah.
MOLA AMSAMEHE MADHAMBI YAKE, AMJAALIE KAULU THABIT NA AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI.
_________________________________________________________________________________________
RAIS DKT. KIKWETE ASIMIKWA UCHIFU WA KABILA LA WABENA MKOANI NJOMBE
Rais Jakaya Kikwete akipokea Mkuki wakati akisimikwa Uchifu
wa Kabila la Wabena na mmoja wa wawakilishi wa Wazee wa Kabila
hilo,kwenye wa Hafla ya Uzinduzi wa Mkoa wa Mpya wa Njombe.
Chifu Mpya wa Kabila la Wabena, Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wakazi wa Mkoa Mpya wa Njombe.
________________________________________________________________________________________
Zanzibar is a
combination of two islands.Thise is Unguja and north of unguja there
Pemba, it people who live in these island is approximately is one
million which are 97% are Muslim, 3%Christian and other pagans
Due to with that approximately we see that most of people who
live in this are Muslim and in case of Muslim in Zanzibar are divided
in to two party these are :-
A) Shia these are all Muslim who believe that there one
god but they don’t believe same calypso like Sayyid Aboubakari, Sayyid
na Omar and they believe Sayyid na Ally
B) Sunni these are all who believe that there one god and Muhammad is prophet of Allah but they believe all calypsos.
Due with that all party live with love each other with out make the joke another due the tradition it has
In case Christian also were divided it two type. Such as:-
A) catholic
B) Pagan
In
party of that Zanzibar was famous country in case religion and
political in the word. in party of donation Zanzibar it was famous
county which help people who got the problem of disease f such as
north America , Tanganyika
And in case of problem of
Muslim Zanzibar was the famous country which help people who was get the
problem that the different country has got the solution of their
problem which has same of them are Uganda ,Kenya ,Sudan, and other
Also
Zanzibar was the center of business in east Africa due to his condition
it has and the different country has desire to established the business
in these islands and also the thing make famous in the word was the
first county to has the taa za barabarani with was use the light gas.
In
party of revolution Zanzibar it has got in January 12, 1964 from the
last sultan sayyid na baraghash and after introduce the multiparty
system in 1992 Zanzibar has lost it quality from other word after happed
conflict of same party. The different agreement happen but nothing
thing has change and the different diplomatic people they came but no
one can make good.
____________________________________________________________________________________
MABOMU NDANI YA DARAJANI
Watu
wasiofahamika bado, usiku wa kuamkia jana Jumatatu walitupa kitu
kinachosadikiwa kuwa bomu lililokuwa katika mfano wa 'sausage' karibu na
eneo la biashara kando ya Barabara ya Darajani mjini Zanzibar.
Msaidizi wa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mkadam Khamis Mkadam akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusu taarifa hiyo alisema, mlinzi binafsi, Amour Kassim Amour (36), aliyekuwa kazini kwenye Duka la Sahara, aliona idadi ya watu katika gari aina ya 'pickup' wakitokea Bwawani kuelekea Mkunazini, walikwenda uelekeo wa dukani alipokuwa akilinda, na walipofika hapo walipunguza mwendo, ndipo mmoja wao aliporusha guruneti upande wake, na kitu hicho kilitua katikati ya masanduku yaliyokuwa mbele ya duka hilo.
"lilikuwa likitoa moshi. Kwa ushujaa, Amour aliliokota na kulitupa mbali na maduka," "Kwa bahati, Amour alilitupa kwenye uwanja wa wazi na hakukuwa na wanunuzi katika mtaa huo wenye shughuli nyingi kwa sababu ilikuwa ni usiku," alisema Mkadam akiongeza kwamba guruneti lililipuka kwa mlipuko wenye sauti kubwa dakika chache baadaye.
Polisi walifanikiwa kupata mabaki ya unga unga na kukusanya kokoto zilizotokana na athari ya mlipuko huo.
Polisi wameanzisha msako na uchunguzi katika tukio hilo, na kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kuripoti kitu chochote kinachoshukiwa

No comments:
Post a Comment