AJIRA

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA ARDHI, MAKAAZI, MAJI NA NISHATI
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi ishirini na moja (21) kwa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kama ifuatavyo:-

1. MINING ENGINEER - Nafasi moja (1) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya ‘Mining’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. ENVIRONMENTALIST - Nafasi moja (1) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza inayohusiana na Mazingira kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. MUHANDISI MIPANGO MIJI – Nafasi moja (1) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya ‘Urban and Rural Planning’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. PETROLEUM ENGINEER – Nafasi moja (1) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Petroleum Engineering kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


5. KARANI MASJALA – Nafasi mbili (2) – UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Utunzaji kumbukumbu kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. KARANI NYUMBA – Nafasi moja (1) – UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya ‘Civil Engineering’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. MLINZI – Nafasi mbili (2) – UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari (Form IV) na amepata mafunzo ya ulinzi kama JKU/Mgambo au yanayolingana kutoka katika taasisi inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8. AFISA SHERIA – Nafasi nne (4) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

9. TAARISHI - Nafasi mbili (2) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari ya kidato cha nne (Form IV) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

10. DEREVA – Nafasi moja (1) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu mafunzo ya udereva kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe na leseni ya Udereva.

11. WAKAGUZI EKA – Nafasi mbili (2) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu mafunzo ya Cheti cha Kilimo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

12. MTHAMINI – Nafasi mbili (2) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya ‘Valuation’ au ‘Uchumi’ kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

13. MCHORAJI – Nafasi moja (1) UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya ‘Catographer au ‘Civil Engineer’ au ‘Survey’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaweza kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini wakati wa saa za kazi.
• Kwa Waombaji walioko Pemba wanaweza kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma iliopo Chake Chake – Pemba.
• Aidha muombaji anatakiwa aanishe nafasi ya kazi anayoiomba miongoni mwa zilizotajwa hapo juu.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo.
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) za Passport Size zilizopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 10 Oktoba, 2014 wakati wa saa za kazi.
N.K. kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya wizara ya utumishi zanzibar www.Lps.go.tz

No comments:

WELCOME TO SEEISSAI BLOG